UZEE KWISHA!!!
Je ulishawahi kutumia Rosela? Kwenye mazingira gani? Kwanini? Katika faida mamia za rosela, basi jifunze hii mojawapo. Rosela ni Anti-aging. Inazuia mikunjo kwenye ngozi. Matumizi ya kila siku ya roselle iliyotengenezwa inaweza kuboresha unyevu wa ngozi na kupunguza mikunjo, kulingana na utafiti kutoka Taiwan. Utafiti mmoja uliofanya chuo kikuu cha Chung Shang, iligundua kuwa matumizi ya kila siku ya 200ml ya kinywaji cha roselle kilichotengenezwa iliweza kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji ya ngozi na kupunguza mikunjo. Utafiti huo uliochukua miezi mitano, ulihusisha takriban watu 60 wenye umri wa miaka 25 hadi 85 kutoka hospitali na mazingira ya jamii. Hii inaweza kuwa kutokana na jukumu la aina mbalimbali za "phytochemicals" zinazopatikana katika maua ya roselle. Utahitaji kuchemsha maua ya Roselle na kunywa maji yake. Baada ya kuchemsha, kemikali zote muhimu zilizopo kwenye Roselle kama vile phytochemicals zitatolewa na kufanya kazi mwilini.