K A S R I
Mfalme Duncan alikuwa akipigana vita kwa takribani miezi sita kwa ajili ya kulinda jiji la Haven. Jiji hili lilikuwa na watu wengi, uongozi wake ulikuwa imara na jeshi lisilopigwa na maadui zake. Wakazi wengi ambao ni wazaliwa na wahamiaji kutoka vijiji jirani, hujishughulisha na shughuli mbalimbali. Ni kijiji tajiri kwa madini na kilimo. Hata hivyo, kutokana na utajiri wa wananchi wake, watoto huzaliwa wakiishi katika mazingira mazuri. Wazee huozesha binti zao kwa kupokea mahari za dhahabu na Vito vingi vya thamani. Hata hivyo, sio rahisi kuingia katika himaya hii ya kifalme yenye sheria kali.
Baada ya kutoka vitani Mfalme aliwaita wake zake watatu; Charlotte , Helena na Victoria pamoja na watoto wake wote ; Elsa, James, Albert, Rose na Belle. Charlotte, aliyevaa gauni refu, la njano, ni mke wa kwanza wa Mfalme Duncan, ana watumishi wapatao mia moja kwa ajili ya kumuhudumia kwa kila atakachohitaji. Charlotte ni mpiganaji vita, aliolewa baada ya baba yake kushindwa vita na Mfalme William ambaye ni baba yake Mfalme Duncan..Charlotte ana watoto wawili James na Belle.
Helena, alivalia gauni jeusi, ana watumishi mia moja na tatu kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali. Anapenda kusoma vitabu.
Helena aliolewa kama mke wa pili baada ya Mfalme Duncan kumuona katika shindano la mabinti wa kifalme la mavazi. Helena alipata watoto wawili ambao ni Albert na Rose.
Victoria , mke wa tatu, alivalia gauni la zambarau, ni mrembo, mchapakazi , na ana mtoto mmoja ambaye ni Elsa. Victoria alikuwa binti wa mpishi katika nyumba ya kifalme. Alikutana na Mfalme wakati akiwapatia askari wa vita chakula baada ya kutoka vitani..Victoria ana watumishi kumi na nne wa kumsaidia shughuli mbalimbali.
Baada ya Mfalme kuitazama familia yake kwa dakika kadhaa, aliwaita vijana wake wa kiume , James na Albert wasogee karibu yake. Aliwaangalia kisha akamgeukia askari wake na kumpa ishara. Askari yule alileta mbele ya Mfalme ubao mkubwa uliokuwa umechorwa ramani.
“Nani aliyewaonesha adui zetu ramani hii"
Vijana waligeukiana kila mmoja akimshangaa mwenzake.
“Kama hamtosema basi siwezi kuwavumilia na kuishi na nyie, kwa sababu mnafki atatuuza muda wowote.........hata hi......."
“Samahani baba, ni Mimi niliitoa hiyo ramani ili maadui wawarudishe kabla hamjafika kwenye himaya yao, kule ni hatari, niliogopa tutakupoteza....." Albert alijibu kwa kutetemeka na kumulikwa na macho ya mshangao kutoka kila pande ya eneo lile.
Bila kuzungumza mfalme alisimama kwa hasira na kumpiga Albert kibao cha nguvu shavuni. Albert alihisi kama sufuria la moto limebandikwa usoni kwa dakika kadhaa. Angeweza kufikiria jinsi ya kula chakula bila kuwa na meno kwani alihisi kwa kipigo kile meno lazima yakose ushirikiano au kung'oka kabisa.
Helena alisogea karibu na kumkumbatia mwanae huku akilia na kumuomba Mfalme angalau amsamehe. Mfalme alitoa amri Albert apewe adhabu kwa siku tatu mfululizo kisha awe huru........
******
Albert akiwa amefungwa kwenye chumba maalumu, James alisogea karibu na kupenyeza macho kwenye giza ili amuone Albert.
“Umefanya vema........ngoja nifikirie jambo jingine utakalofanya. Usivunje masharti.........." James alimwambia Albert kisha akageuka ili aondoke....
“Waambie hiyo siri, sipo tayari kuteseka na kuonekana mbaya kwa baba yangu kwa sababu yako...utanilazimisha nikubali mambo ya uongo mpaka lini?." Albert ambaye alikuwa amesimama akishikilia chuma za dirisha alifoka kwa hasira.
James alirudi na kumsogelea kwa karibu zaidi.....“Upo tayari niseme siri? Upo tayari kwa matokeo? Upo tayari Mfalme agundue kwamba wewe sio mtoto wake? Na kwamba mama yako alikuiba kwa binti maskini ili apate mtoto wa kiume wa kurithi ufalme? Sawa muda si mrefu utakuwa huru, ila pia utafukuzwa ndani ya himaya hii ya kifalme......." James aliacha mzungumzo na kuondoka.
“Subiri.....Albert aliita...“Usimuambie mtu yeyote kuhusu suala hilo. Nitakusikiliza wewe..."
..................pata riwaya hii ndefu na yenye kuburudisha kwa shilingi elfu Tano tu Kwa pdf (softcopy).........
Comment ukihitaji.
Karibu sana.

Comments