Super Morsa
Uwiiiiii aiiiiiiii jaman nakufaaaaa........Alora alilala chini akiugulia maumivu makali kutokana na kipigo cha mumewe Chiumbo. Mlango ulikuwa umefungwa, hakuna jirani aliyeweza kumwokoa Alora. Aidha tegemeo la pekee lingekuwa mtoto aliyeko tumboni, ambaye Alora humwimbia nyimbo na kumsihi awahi kuzaliwa ili Alora apate rafiki.Alora aliugulia maumivu makali kila kona ya mwili wake. Aliikinga mikono yake tumboni ili mateke ya Chiumbo yasimdhuru mtoto.Chiumbo alipochoka kumpiga Alora mateke, alianza kumpiga na kila alichokiona mbele yake.Alimpiga kila sehemu. Alora sio mda alianza kuona giza, aliona kila kitu kilichomzunguka kinabadilika na kuwa cheusi. Alianza kulegea hadi kulala chini kabisa. Alizimia. Chiumbo aliyekuwa anayumba huku na kule kwa pombe kali kichwani alifungua mlango na kutoka nje. Alichukua ndoo ya maji na kwenda kumwagia Alora mwili mzima. Alora alifungua macho haraka kama mtu aliyetoka kwenye usingizi wenye ndoto mbay...