Super Morsa
Uwiiiiii aiiiiiiii jaman nakufaaaaa........Alora alilala chini akiugulia maumivu makali kutokana na kipigo cha mumewe Chiumbo. Mlango ulikuwa umefungwa, hakuna jirani aliyeweza kumwokoa Alora. Aidha tegemeo la pekee lingekuwa mtoto aliyeko tumboni, ambaye Alora humwimbia nyimbo na kumsihi awahi kuzaliwa ili Alora apate rafiki.Alora aliugulia maumivu makali kila kona ya mwili wake. Aliikinga mikono yake tumboni ili mateke ya Chiumbo yasimdhuru mtoto.Chiumbo alipochoka kumpiga Alora mateke, alianza kumpiga na kila alichokiona mbele yake.Alimpiga kila sehemu. Alora sio mda alianza kuona giza, aliona kila kitu kilichomzunguka kinabadilika na kuwa cheusi. Alianza kulegea hadi kulala chini kabisa.
Alizimia.
Chiumbo aliyekuwa anayumba huku na kule kwa pombe kali kichwani alifungua mlango na kutoka nje. Alichukua ndoo ya maji na kwenda kumwagia Alora mwili mzima.
Alora alifungua macho haraka kama mtu aliyetoka kwenye usingizi wenye ndoto mbaya. Gafla alivutwa mkono na kusukumiwa mlangoni. Aligonga kichwa chake kwenye kitasa cha mlango wa chumba chake akapoteza tena fahamu. Chiumbo alisogea kando ya kitanda na kuchukua chupa yake ya pombe kisha akaondoka na kumwacha Alora pale chini.
*******************
Masaa kadhaa baadae Alora aliamka na kujikuta kazungukwa na vyombo, maji yamemwagwa chumbani mwili unamuuma na hawezi kusimama. Akajishika na kitasa hadi alipoweza kusimama lakini alidondoka chini. Alitambaa hadi alipofika kwenye kitanda chake kisha akajivuta na kujilaza kitandani. Macho yalikuwa mazito, na mekundu. Akili yake iliwaza mengi na wala hakuwa na msaada.
Gafla alishika tumbo lake, maumivu makali yasiyoelezeka. Mgongo wake ulikuwa kama anachomwa sindano, alianza kulia huku akijitahidi kusimama kutoka nje. Alora alipiga kelele za msaada lakini kama masaa kadhaa yaliyopita wakati akipigwa, hakupata msaada. Alora aliishiwa nguvu akadondoka chini.
Alihisi roho yake inataka kutoka kutokana na maumivu yale. Alora alikuwa anapata uchungu. Hakuwa na msaada. Baada ya kipigo kizito kutoka kwa mume wake asiyejali, sasa alikuwa anapitia tena uchungu bila kuwepo kwa msaada wowote.
Kukosa msaada kulimuogopesha Alora. Miguu yote ilikuwa imevimba kwa kupigwa. Mikono yake ilikuwa kama imefungwa tani elfu moja za chuma. Alora kwa shida alimvuta mtoto kichwa kwa kujikaza akiwa pale chini. Alihisi kushindwa ila alijua akishindwa kufanya ivyo atampoteza mtoto pamoja na yeye.
Baada ya dakika chache Alora alishindwa kuamini kwamba aliyembeba mkononi ni yule rafiki yake aliyekuwa amembeba tumboni, waliyekuwa wanafuatana kila mahali. Pamoja na Alora kuishiwa nguvu, alihisi furaha ya ajabu kisha akaanza kulia. Alifikiria dunia ilivyo katili na jinsi mwanae huyo ataenda kukutana na watu wasio na huruma.
Alora alijisogeza hadi kwenye vyombo. Alichukua kisu na kukata kitovu cha mwanae. Alimwangalia tena usoni akasema “Raza, litakuwa jina lako. Kwa sababu umenipa matumaini na utakuwa faraja kwangu siku zote. Nitakuwa shujaa wako popote uendapo"
Baada ya kuzungumza hayo Alora alihisi nguvu za mikono zinamwishia. Alimnyanyua mtoto hadi alipoweza kumweka kitandani huku Alora akiwa pale chini. Alora alishindwa kufanya chochote kwani alihisi mwili sio wake kutokana na maumivu kila sehemu. Mtoto alikuwa akilia kwa sauti kubwa. Alora alianza kuisikia sauti ya mwanae kwa mbali sana hadi pale ilipofifia na kutosikika kabisa.
************************
Alora aliangalia pande zote bila kuona mtu. Alikuwa katika chumba ambacho sio kigeni kwake. Ila alikuwa hakumbuki ni wapi hasa. Gafla aliamka na kuanza kulia...
“Raza wangu jaman....jaman Raza wangu yuko wapi......Jaman nipo wapi hapa....." Alora alilia huku akijigeuza kwenye kitanda kidogo alichokuwa amelala. Katika harakati za kujigeuza alianguka chini.. Alitulia pale chini kwa dakika kadhaa akakumbuka muda fulani alimbeba mtoto mkononi...“Raza wangu" ....Alora alishindwa kukumbuka nini hasa kiliendelea....
Mda kidogo alisikia hatua za mtu zinamkaribia. Alipogeuka alimuona mwanamke mrefu akiingia ndani huku amebeba mtoto. “Ayanna,....." Alora aliita huku akijitahidi kunyanyua kichwa.
“....Ayana namuomba mwanangu....... Mwanangu anaendeleaje......" Alora alimwita wifi yake baada ya kumgundua tu alipomuona sura yake.
“Hustahili kuishi. Wewe ni mwanamke mbaya sana. Unataka kumuua huyu mtoto makusudi? Kwanini usingewahi hospitali hadi ukajifungua nyumbani tena peke yako?....." Ayana aliongea kwa ukali huku akimweka mtoto pembeni ili amnyanyue Alore pale chini.
“Aiiiii taratibu Ayanna. Mwili unauma sana. Kaka yako amenipiga sana......ameniumiza ......" Alora aliongea kwa shida huku akishindwa kuhimili maumivu aliponyanyuliwa kwanguvu na Ayanna.
“Kaka yangu hapigi mtu bure....hata kama ningekuwa mimi ningekupiga. Mwanamke mjinga sana wewe....." Ayanna aliongea kisha akamchukua mtoto na kumpeleka kwa Alore. “Nilikusikia ukilia ila nikasema ni mke anafundishwa adabu na mumewe, kama sio sauti ya mtoto basi usingeniona hapa sasa hivi. " Ayanna alimkabidhi mtoto kwa Alore kisha akaondoka bila kuongeza neno.
“Ayanna.... Ayanna...." Alore aliita bila kuitikiwa. Alimwangalia mwanae akaanza kulia kwa majonzi makubwa. “Samahani mwanangu.....mama anakupenda....hataki ufe" Alora alilia sana huku maneno ya Ayanna yakijitafsiri akilini na kumfanya ajione yeye sio mke wala mama bora kwa Chiumbo na Raza.
********************
Miezi kadhaa baadae, Chiumbo alirudi nyumbani baada ya kutokomea kusikojulikana kwa muda mrefu. Alikuwa kanenepa, kanawiri lakini alionekana ana mawazo.
“ Pole na safari......" Alore aliongea bila kumwangalia mumewe usoni huku akiendelea na kazi zake.
Chiumbo alimuangalia Alore kwa dakika kadhaa kisha akamsogelea.
“ Mke wangu, nakupenda sana. Najua nilichokufanyia mara ya mwisho siyo kizuri. Naomba unisamehe. " Chiumbo alimshika mkewe mkono huku akimuelekeza waelekee chumbani.
“Nimepoa tayari. Ulikuwa wapi siku zote...." Alore aliachanisha mikono huku akiongea kisha akatangulia chumbani. Chiumbo alimfata mkewe lakini kabla hajafika, alimuona mkewe amembeba mtoto mchanga akitoka naye nje. Chiumbo alimuangalia Alora bila kupepesa macho. Alishangaa kwa kile anachokiona kwani tokea aondoke alisahau kwamba mkewe alikuwa mjamzito.
Alore alivofika mlangoni Chiumbo alimkumbatia huku akijuta....
“Nisamehe sana mke wangu. Nimekuwa baba mbaya sana na mume mbaya ambaye hata sistahili kuishi. Nimekutesa sana mke wangu. Hakika wewe ni mvumilivu sana. Sitarudia nilichokufanyia........"
Alore alimwangalia mume wake huku akitamani aondoke akae nae mbali kwani alifikiria yaliyomtokea na shida alizopitia jinsi zilivomfanya awe dhaifu katika nafsi yake.
“Niahidi kwamba umenisamehe mke wangu na hautonichukia" Chiumbo aliendelea kulalamika hadi Alore alipofungua mdomo......
“Chiumbo, siku ya kwanza kuishi na wewe ulikuwa mwanaume bora sana kwangu. Niliona dunia yote ni yangu. Lakini kwa sasa sitamani tena ndoa hii iendelee kwa uliyonifanyia. Nimeteseka sana."
Chiumbo alimbeba mtoto kisha akasema “ Najua nimeivunja imani yako ya ndoa hii. Lakini nakuahidi mimi sitakunywa pombe tena wala sitakupiga mke wangu. "
“Sawa....." Alore aliitika kisha akamchukua mtoto na kutoka nje.
********************
Maisha yalikuwa mazuri. Raza alionja upendo wa baba na mama na kwa furaha familia ilinawiri.
Msamaha ulikuwa umetawala na kila mmoja alikuwa amemkumbuka mwenzake. Wote walihisi upungufu fulani katika kipindi ambacho hawakuwa pamoja. Alore alianza kutabasamu tena. Alisahau mateso yote yalipita na kuanza kuona nuru mpya katika ndoa yake.
“ Alore, wewe ni mwanamke bora sana. Sijui nilikuwa na sifa gani kukupata mwanamke mzuri kama wewe......" Chiumbo alimnong'oneza Alore.
Alore alitabasamu kiasi cha kuzidi kumchanganya mumewe huyo ambaye alionekana na kiu ya kukutana na mkewe baada ya kuwa mbali nae kwa muda mrefu.
Usiku ulikuwa mfupi sana kwa Chiumbo na Alore huku wakistaajabu kwanini muda wa raha huwa mfupi kuliko muda wa karaha.
Chiumbo alimsifia mkewe, alimwita majina mengi mazuri na kulifufua upya tabasamu la Alore lililokuwa limepotea kwa muda mrefu.
************
“Unaenda wapi bado ni mapema sana" Alore aliongea kwa uchovu huku akijikuna macho yake kutoka usingizini.
“Nitarudi, kuna sehemu ya muhimu naenda........" Chiumbo alikwishaoga na alikuwa akijiandaa kuondoka bila kusema atakapoenda.
“Ila ulisema unataka ukae na mtoto hadi akuzoee. Na pia ....." kabla Alore hajaongea Chiumbo alidakia....
“Mimi ni mwanaume siwezi kaa ndani. Tena na mtoto? We mwanamke haupo serius. Huyo ni mtoto wa kiume. Sio lazima akue akiona ona sura ya baba."
“Sawa....... Uwe na siku njema. Hata hivyo najua hutorudi
......" Alore alimuaga mumewe huku akigeuka upande wa pili wa kitanda na kulala
Chiumbo ambaye alikuwa hajamuangalia mkewe usoni sasa aligeuka na kumuomba arudie alichosema.
“Hii ndio tabia yako mume wangu, sijawahi kukuelewa. Hata sasa najua ulikuja kunidanganya tu" Alore aliketi baada ya kumuona mumewe amebadilika....alijua kitakachofuata. Yote alivumilia.
Miaka ilizidi kwenda Alora akivumilia mambo yote anayofanyiwa, aliendelea kumlea mtoto wake katika hali zote hadi alipokuwa mkubwa. Hali ilikuwa mbaya kwake.
************************####### miaka michache baadae.
Mama yake Chiumbo pamoja na dada yake, Ayanna, walikuwa wametulia wakishangaa jinsi Alora anavyopigwa. Alora alikuwa ametolewa nje huku akiwa na khanga tu. Aliburuzwa chini jambo lililompelekea kupata mikwaruzo kadhaa.
Ni miaka kadhaa na michache sasa lakini Alora alikuwa amepoteza nuru usoni. Alikosa matumaini. Alikuwa anachekwa kila wakati.
Mume wake alikuwa bondia kwa mkewe. Mara kadhaa Alore alipoteza ujauzito kutokana na vipigo vya mume wake.
Alore alibaki kugugumia maumivu ya kipigo na vicheko kutoka kwa ndugu wa mume wake.
Alibaki pale nje akiwa analia, mwili ukiwa mzito asiyeweza hata kusimama.
Alibaki pale chini kwa dakika kadhaa. Alifikiria ndoa ilivoanza na nuru, na sasa mbele kulikuwa na giza tu.
Alikuwa na ndoto nyingi lakini zote zilitokomea kutokana na mume wake.
Alore aliona kivuli kando yake, aliona maji yakidondoka kwenye mikono yake. Aliinua uso kujua ni nini hasa kilichokuwa kinatiririsha maji yanayoangukia mkononi mwake...........!
*****************
Alore alipoangalia vizuri alimuona kijana mrefu na mtanashati anamuangalia. Kijana yule alimuinua Alore na kumkumbatia. “ Pole mama".
Alore aliangua kilio baada ya kusikia pole ile......hakuna mtu yeyote aliyewahi kumuambia pole wakati anaumia.
“Tumaini langu, Raza wangu....." Alore alimwangalia kijana wake kwa kulia.
“Mama, miaka yote wewe unapigwa tu, huchoki? Kwanini unapigwa? ...." Raza alimuuliza mama yake..ila kabla hajapata jibu, bibi yake alimwita. Raza alimsaidia kwanza mama yake kisha akaenda kwa bibi.
“Raza, we ni kijana mkubwa sasa. Najua umeshuhudia jinsi mama yako anavyopigwa kila wakati. Hivi unadhani baba yako ni mbaya?" Bibi Raza aliuliza huku akimpakulia Raza chakula aliyeonekana ana njaa.
“Ndiyo bibi, baba ni mbaya sana. Anampiga mama kila wakati..." Raza aliongea na kupokea chakula alichopewa.
“Kuna kitu nataka leo ujue. " Bibi aliongea kisha akamsogelea Raza karibu. “Mama yako ni mchawi..mara kadhaa amejaribu kukuua ndio maana baba yako anampiga. Najua hawawezi kukwambia ukweli..ila ukweli ndio huo. "
“Hapana bibi, mama sio mchawi......" Raza aliongea na kuweka chakula chini ili atoke nje lakini alikutana na Ayanna mlangoni.
“Kwahyo mama yako anapigwa bure? Unashindwa kujiuliza kwanini majirani hawamtetei mama yako? Anataka kukuua. " Ayanna alidakia huku akimpisha Raza atoke nje.
Raza alishindwa kuamini. Alikaa siku nzima akitafakari aliyoyasikia. Lakini aligoma kuamini. Aliwaza sana hadi akaishia usingizini akiwa ameketi nje peke yake.
“Aiiii mama nyoka, nyoka....." Raza alishtushwa na maumivu makali na alipoangalia alimuona nyoka akitokomea.. Alipokuwa anapiga kelele Alora alikuja haraka kumuokoa mwanae....... Wakati akimpatia huduma, Ayanna na mama yake/ bibi Raza walikuja kuona nini kinaendelea.
“Hahhaahha kwanini unamchukia huyo mtoto sana..." Ayanna alizungumza kisha akamvuta Raza, “Huyo nyoka aliyekunga'ta ni mama yako kamtuma. Ndio maana mtaa mzima unamuogopa huyu mama yako.....na tunafanya uchunguzi tujue huwa anamficha wapi....."
Kabla Ayanna hajamaliza kuongea alishtukia kofi zito usoni. Alore alikuwa na hasira, alimvuta Ayanna bila kuongea na kuanza kumpiga. Ayanna alipiga kelele. Bibi Raza nae akamsaidia Ayanna. Wote kwa pamoja wakaanza kumpiga Alore. Raza aliishiwa nguvu. Maumivu ya mguu yalizidi. Alidondoka chini jambo lililofanya kila mtu aache kupigana na kumrukia Raza.
“Raza mwanangu.....Raza....." Alore alimbeba Raza na kukimbia kumuita muuguzi.
Masaa kadhaa baadae Raza aliamka na kumkuta mama yake ameketi kando analia.
“Mama....niambie ukweli, kwanini kila mtu anakuita mchawi...."
“Kwa sababu wananichukia....."
“Kwanini wakuchukie wewe tu...."

Comments