KASRI 2
"Hapana Albert, ukiondoka kila kitu kitajulikana......naweza kunyongwa kwa kosa la kumdanganya mfalme kwa miaka yote hiyo....." Helena alisimama akimsihi Albert asiondoke huku akiwa ameushika mkono wake..... Kimya kilitawala kidogo ambapo Albert na Helena walisikia kama nguo ikikwaruza ukuta, ilikuwa ni kama mtu aliyejibanza na ukuta akijaribu kusogea mbali baada ya kusikiliza mazungumzo yale. Albert alizunguka nyuma ya ukuta ule kulipokuwa na chumba cha stoo kisha akamdaka mtu aliyekuwa kwenye harakati za kunyata ili aondoke eneo lile. “ Tulia hapo, we ni nani....".Albert alimuuliza na kabla hajapewa jibu alimtambua mtu yule kwamba ni James, mtoto wa mke wa kwanza wa mfalme. Albert aliuachia mkono wa James huku akishangaa kwa hofu akijua kwamba siri kubwa imejulikana... “ Wewe umefata nini hapa, umesikia kitu gani.. " James bila kuzungumza chochote aliondoka akimkata Albert jicho kali. Albert aligeuka na kumfuata Helen ambaye kwa wakati huo alikuwa amejibanza ukut...